Na Alfred S. Mbonye,
Idara ya Mawasiliano, Jimbo Kuu la Mwanza.
Baba Mtakatifu Leo XIV, tarehe 11 Novemba 2026 amemteuwa Mheshimiwa Sana Padre Maximiliani Francis Buluma wa Jimbo Kuu la Mwanza kuwa Askofu msaidizi wa Jimbo kuu la Mwanza, nchini Tanzania. Hadi kuteuliwa kwake Askofu msaidizi Maximiliani Francis Buluma alikuwa ni Gambera wa kwanza wa Seminari kuu ya Mtakatifu Mikaeli, Jimbo kuu la Mwanza na kabla ya hapo alikuwa ni Jaalimu na Mlezi wa Seminari Kuu ya Mtakatifu Augustino, Peramiho, Jimbo kuu la Songea, Tanzania. Itakumbukwa kwamba, Askofu msaidizi Maximiliani Francis Buluma alizaliwa tarehe 29 Oktoba 1976, jimbo kuu la Mwanza, Tanzania. Baada ya masomo na majiundo yake ya Kikasisi tarehe 10 Desemba 2006 akapewa daraja takatifu ya Upadre kwa Jimbo kuu la Mwanza. Tangu wakati huo, amehudumia kama Paroko-usu Parokia ya Mtakatifu Bernadetta, Kahangala kati ya Mwaka 2006-2007; Paroko wa Bikira Maria Mama wa Wamisionari, Malya kati ya Mwaka 2007 hadi 2008.
Kati ya Mwaka 2008 hadi 2009 aliteuliwa kuwa Katibu muhtasi wa Askofu mkuu wa Jimbo kuu la Mwanza. Baadaye alitumwa nchini Italia kujiendeleza kwa masomo ya juu kwenye Chuo Kikuu cha Kipapa “Pontificia Facoltà Teologica dell’Italia Meridionale, Sezione San Tommaso d’Aquino” Cha Mtakatifu Thomas wa Akwino, kati ya mwaka 2009 hadi mwaka 2015 na kujipatia Shahada ya Uzamivu katika masomo ya: “Christology.” Baadaya ya kurejea nchini Tanzania alipangiwa kuwa Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Karoli, Ibindo kati ya Mwaka 2015 hadi 2016; Gambera wa Sekondary ya Wasichana ya Askofu mkuu Mayala Ibindo kati ya Mwaka 2015-2016. Baadaye aliteuliwa kuwa Gambera wa Seminari Ndogo ya Nyegezi kati ya Mwaka 2016-2017. Na Jaalimu na Mlezi wa Seminari Kuu ya Mtakatifu Augustino, Peramiho, Jimbo kuu la Songea kati ya Mwaka 2016 hadi mwaka 2017. Baba Mtakatifu Leo XIV, tarehe 11 Novemba 2026 akamteuwa Mheshimiwa Sana Padre Maximiliani Francis Buluma wa Jimbo Kuu la Mwanza kuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo kuu la Mwanza.
Ajouter un nouveau commentaire