• archmwanza@gmail.com
  • +255 769 523 036

Upadrisho Sahwa

Upadrisho Sahwa

Posted on: 01 Aug, 2024

Kuelekea adhimisho la Misa Takatifu ya Upadrisho katika Parokia ya Mt. Bathromeo - Sahwa

HISTORIA YA SHEMASI

NELSON MINZANI TIZOLEKEZA

A: KUZALIWA: Nelson Minzani TIZOLEKEZA alizaliwa tarehe 20 April 1994 katika Kijiji cha Kashenge (Kilembo), Kata ya Katoma – Bukoba, Kagera. Ni mtoto wa sita kati ya Watoto sita wa Baba Petro Paulo Rugaimukamu (marehemu) na Mama Joanna Maria Kokubanza.

B: IMANI KATOLIKI

UBATIZO: Alibatizwa Desemba 28, 1994 katika Parokia ya Mtakatifu Yohane Mbatizaji- Katoma, Jimbo Katoliki la Bukoba. Namba ya Ubatizo ni LB 4084.

KOMUNYO YA KWANZA: Desemba 28, 2000 katika Parokia ya Mtakatifu Yohane Mbatizaji- Katoma, Jimbo Katoliki la Bukoba.

KIPAIMARA: June 11, 2006 katika Parokia ya Mtakatifu Yohane Mbatizaji – Katoma, Jimbo Katoliki la Bukoba.

C: ELIMU: Shule ya Msingi Katoma “B” (2001-2008), 2009 -2012 Seminari ya Mtakatifu Maria – Rubya Seminary iliyoko Jimbo Katoliki la Bukoba, Omumwani Sekondari na baadae Sekondari ya Geita kidato cha V & VI (GESECO 2013-2015).

D: SAFARI YA MALEZI YA WITO WA UPADRE:

Juni – Septemba 2015 Nyumba ya Malezi ya Mt. Yohane Paul II, Kawekamo – Jimbo Kuu la Mwanza.

2015 – 2018: Masomo ya Falsafa katika Seminari Kuu ya Mt. Anthony wa Padua, Ntungamo – Bukoba. 29 Novemba, 2015 alivikwa rasmi Kanzu, Ntungamo Seminari na Mha. Desderius Rwoma, Askofu Mstaafu wa Jimbo Katoliki la Bukoba.

2018-2023: Masomo ya Tauhidi (Teolojia) katika Seminari Kuu ya Mt. Karoli Lwanga, Segerea – Dar es Salaam. 2019 alipewa Huduma ya Usomaji, Segerea Seminary- Dar es Salaam na Mwadhama Kardinali Polycarp Pengo. 2020 alipewa huduma ya Utumishi Altare, Segerea Seminary- Dar es Salaam na Mha. Renatus L. Nkwande, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Mwanza.

Julai – Novemba 2023: Mwaka wa Kichungaji, Nyumba ya Baba Askofu Mkuu, Kawekamo.

Kuanzia Novemba 2023 hadi sasa, anaendelea na Masomo katika Chuo Kikuu cha Mt. Agustino (SAUT- MWANZA).

E: UTUME:

2016 – Parokia ya Buhingo.

2017 – Parokia ya Mt. Yustino - Bujora.

2018 – Parokia ya Mt. Francisko wa Asizi - Mbalika.

2019 – Parokia ya Kung’ara Sura kwa Bwana Wetu Yesu Kristo - Mabatini.

2020 - Parokia ya Kung’ara Sura kwa Bwana Wetu Yesu Kristo – Mabatini.

2021 – Parokia ya Mbalika na Nyumba ya Baba Askofu, Kawekamo.

2022 – Nyumba ya Baba Askofu, Kawekamo.

Daraja ya Ushemasi: Januari 06, 2024, Kituo cha Hija Kageye (Parokia ya Kayenze) na Mha. Liberatus Sangu, Askofu wa Jimbo Katoliki la Shinyanga.

Anawashukuru watu wote waliomsaidia katika safari ya masomo na malezi hadi kuifikia sikuu hii anapoijongea Altare ya Bwana. Anaomba tuungane naye na kusali pamoja naye leo anapotarajia kupewa Draja Takatifu ya Upadre ili Mungu amjalie uthabiti katika utume wake. Anaongozwa na maneno ya Nabii Isaya “Mimi hapa, Nitume mimi Bwana(Isaya 6:8).



HISTORIA YA SHEMASI

GRAYSON WILBROAD RUTAJUMBUKILWA

KUZALIWA:

Grayson Wilbroad RUTAJUMBUKILWA alizaliwa March 15, 1991 Nyamagana-Mwanza (Tanzania). Ni mtoto Wa tatu kati ya watoto watano Wa Baba Wilbroad William Rutahiwa na mama Hildagardas Protas.

IMANI KATOLIKI

Shemasi alibatizwa na kupata komunio ya kwanza 25-12-2002 katika Parokianya Kristo Mfalme Nyantakubwa-jimbo la Geita. Namba ya ubatizo ni 1984.

KIPAIMARA: June 20, 2004, parokia ya Yesu Kristo Mfalme Nyantakubwa- Jimbo la Geita, na Mha. Askofu Damian Denis Daru. NB 10920.

ELIMU:

1998-2005: Shule ya msingi

2006-2007: Mwaka Wa malezi Sayusayu -Shinyanga

2007-2010: Seminari ndogo ya Makoko-Mara

2011-2013: high school Mwenge -Singida

SAFARI YA MALEZI YA WITO WA UPADRI:

2013-2014: Malezi ya uasipiranti -nyumba ya malezi ya wamisionari Wa Konsolata-Morogoro

2014-2017: Masomo ya falisafa -chuo kikuu Cha Jordan -Morogoro

2017-2018: Malezi ya unovisi- Sagana -Kenya

07, 07, 2018: Nadhiri za kwanza-Sagana Kenya. Na mkuu Wa shirika regione ya Kenya (Joseph Waithaka)

2018-2019: Malezi na mafunzo ya Lugha (kiitaliano), mila na desturi- Roma-Italia

2019-2022: Masomo ya teolojia (tauhidi)-Urbaniana

06,07, 2023: Nadhiri za Daima na mkuu Wa shirika regione ya Ulaya (John Treglia)

08, 12, 2023: Daraja ya ushemasi Jimbo kuu la Torino (Italia) na Mha. Askofu mkuu Roberto Repole.

2022-2024: masters katika uchungaji (masters in Pastoral theology)-Chuo kikuu Cha wasalesiani-Torino-Italia

UTUME:2013-Parokia ya Nyantakubwa- Geita; 2014 parokia ya Mkundi -morogoro; 2014-2017-Parokia ya Kasanga Morogoro; 2017-2018 kigango Cha Mitundu-Sagana (Kenya); 2018-2019: parokia ya Mt Paulo Wa msalaba -Roma; 2020-2022: parokia ya Mt. Jerome-Roma; 2022-2024 Parokia ya Mt Joseph Kafaso-Torino+ utume kwa jumuia ya wahamiaji kutoka Naijeria wanaoishi Torino (Italia).

Shemasi anatualika tusali pamoja naye leo 08,08, 2024 anapotarajia kupewa daraja takatifu ya Upadri, ili mungu amjalie kuwa imara katika kumtumikia, awe mwana wa Amani katika kulihudumia Kanisa Kwa namna zote.(Yohane 14:27).

Tutto per un solo obiettivo “ la santità in Cristo Gesù

Everything good accomplished for only one goal “holines in Christ Jesus “

Yote Kwa lengo Moja ‘tu’ “Utakatifu katika Kristo Yesu”

Share This


Comments (0)

No Comment Found

Post Your Comment