Parish Details
HISTORIA
FUPI YA PAROKIA YA MTAKATIFU BARTHOLOMEO - SAHWA
Parokia ya Mt
Bartholomeo Sahwa ilianzishwa kama kigango mnamo mwaka 1994 na kuwa ni miongoni
mwa vigango vilivyokuwa sehemu ya Parokia ya Nyegezi, chini ya Paroko Pd. Peter
Mwanjonde na Katekista aliyehudumu wakati huo alikuwa ni Renatus Zephania
ambao kwa sasa wote ni marehemu.
Mnamo mwaka 2007
baada ya Kigango cha Mt. Augustino Mkolani ambacho kilikuwa miongoni mwa
vigango vya Parokia ya Nyegezi kupewa hadhi ya kuwa Parokia, Kigango cha Mt.
Bartholomeo - Sahwa kiliwekwa chini ya Parokia ya Mkolani. Mwaka
2016 Parokia ya Mt. Monica Buhongwa ilizinduliwa, ambapo Kigango cha Mt.
Bartholomeo Sahwa kilikuwa sehemu ya vigango vinne vilivyounda Parokia ya Mt.
Monica Buhongwa, vigango vingine vilikuwa: Kigango Mama cha Mt. Monica
Buhongwa, kigango cha Mt. Isdori Bulale ambayo kwa sasa ni Parokia ya Huruma ya
Mungu Bulale na Kigango cha Mt. Yohane Chrisostom Lwanhima.
Mnamo tarehe 7
July mwaka 2018 Baba Askofu Mkuu Yuda Thaddeus Ruwa'ichi, wakati wa ziara yake ya
kichungaji katika Parokia ya Mt. Monica Buhongwa, alitangaza kukipandisha
hadhi kigango cha Mt. Bartholomeo Sahwa kuwa Parokia Teule chini ya
Parokia ya Mt. Monica Buhongwa, huku kikiwa chini ya usimamizi wa Baba Askofu
Mkuu Yuda Thaddeus Ruwa’ichi na Paroko Msaidizi akiwa Pd. Festo Ndiu –
OSA. Mwaka 2019 Parokia ya Buhongwa ilipata Paroko mpya Pd. Gontardo
Fidelis Matavika - OSA, akisaidiwa na Pd. Athanas Edward Zengo - OSA, na baadae
alifika Pd. Edgar Mlelwa - OSA kuwa Paroko Msaidizi, ambaye naye alihamishwa na
kuja Padre Xavery Masanja OSA. Mwaka huu mnamo mwezi June Parokia ya Mt.
Monica na Parokia Teule ya Bartholomeo Sahwa tulipata Paroko mpya, Pd.
Afrates Luambano - OSA, na Paroko Msaidizi Pd. Erasto Mgani – OSA ambao walitulea
mpaka tuliposimikwa rasmi kuwa Parokia na kuwa chini ya Padre Joseph Ndalahwa
kama Paroko wa kwanza wa Parokia ya Mt. Bartholomeo Sahwa.
Pia kwa namna ya
pekee tunawashukuru mapadre mbalimbali waliotuhudumia kwa nyakati tofauti
wakiwemo; Pd. Edgar Ngowi - OSA, Pd. Benard Mlowe – OSA, Pd. Joel Nziku - OSA,
Pd. Ephraem Msigala - OSA, Pd. Cyril Mlupi - OSA, Pd. Partrick
Mpoli, Pd. Ibrahimu Ngassa, Pd. George Nima Nzungu, Pd. Akriatus
Thobias, Pd. Bernadin Mtula, Pd. Basil.P.Rwezaura - OSB, Pd. Carlo J. Mwalongo,
Pd. Deogratius Katai, Pd. Demitrius Njiku, Pd. John Makungu, Pd. Evarist
Charahani, Pd. Fabian Ngeleja, Pd. Joseph Jamhuri, Pd. Engeibert Nyandwi, Pd.
Paul Ngayomela, Pd. Seletine Nyanda na Pd. Moses Mapera na mapadre wengine
kutoka Chuo Kikuu cha Mt. Agustino (SAUT) Mwanza, Chuo Kikuu cha Sayansi
Bugando (CUHAS), mapadre wa shirika la Mt. Agustino na jimbo kuu la
Mwanza kwa namna moja au nyingine ambao wamekuwa msaada kwetu wakati
wote. Tunasema asanteni sana.
Tunamshukuru Mhashamu Baba Askofu Mkuu Jude Thaddaeus
Ruwa’ichi ambaye aliona hitaji na kutupatia hadhi ya Parokia Teule
07.07.2018. Mungu ambariki.
Aidha, kwa namna ya pekee tunakushukuru sana Mhashamu Baba
Askofu Mkuu Renatus Leonard Nkwande kwa maongozi yako mbalimbali katika
kulijenga Kanisa la Mungu, ambayo wakati wote yamekuwa ni dira na msaada mkubwa
katika maendeleo ya Parokia hii hadi kufikia siku ya leo. Hakika sifa na
utukufu ni kwa Mungu wetu Katika Kristo Yesu kwa ajili yako na Kanisa kwa
ujumla kwetu.
Pia hatutawasahau makatekista waliowahi kuhudumu mahali
hapa na wanao endelea, Katekista Renatus Zephania ambaye ni marehemu, Katekista
Meshack E.Ndaki, Katekista Elias Katemani, Katekista Yohane Masinde, na
makatekista wanao endelea kutuhudumia hadi sasa, Katekista Paskali Luchapa na
Katekista Lidya Kokunyegeza.
Kigango kilipitia awamu mbalimbali za uongozi wa
Halmashauri walei mpaka inakuwa Parokia Teule na kwa sasa viongozi wa
Halmashauri walei ni hawa wafuatao:
Michael Daniel
Masimbani………… Mwenyekiti
Rosemary Agustino
Gesura………... Makamu mwenyekiti
Emmanuel Muhangwa
Daud ……… Katibu
Nice Ernest
Kanyabuhula………….. Katibu msaidizi
Rosada Paul
Msaki………………… Mhazini
Asanteni kwa
Huduma yenu na Mungu awabariki sana.